Hatimaye Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuaishi katika matesa makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed Omary. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria  kutoa hukumu inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha Nasra.

 Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.
  Mbunge Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
 Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.

  Mazishi ya mtoto Nasra yaliendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
  Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 'INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUN' Mwenyeez Mungu mrehemu Yaa Arhama R'rahimin mja wako huyo asiye na hatia yeyote, Malaika wa Mungu,' Mpokee na mughufirie kwa yote, umpumzishe palipo pema peponi, mnusuru na adhabuzo zote za duniani, za kaburini na kesho akhera. Mjaaliye kila jema na awe ni miongoni mwa waja wako wema utakaowaingiza katika yako JANNATU N'NAEEM kesho Yaumul Hisabu. - AMEEN. Pumzika palipo pema Nassra, uliteseka si hab

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...