Mshambuliaji Oribe Peralta wa Mexico amehakikisha kwamba haki inatendeka katika michezo ya awali ya Kombe la dunia alipoiwezesha nchi yake kuifunga Cameroon bao 1-0 jioni huu mjini Natal wakati michuaono hiyo ikiwa katika hatihati ya kashfa ingine ya uamuzi mbovu.
Endapo kama Mexico wasingeshinda ni hakika Refa huyo kutoka Colombia Wilmar Roldan angekuwa katika wakati mgumu baada ya kukataa magoli mawili ya wazi ya timu hiyo kwa madai kuwa ni ya kuotea baada ya mchezaji wa zamani wa Tottenham Giovani dos Santos kutingisha nyavu za Cameroon mara mbili katika kipimdi cha kwanza.
Ndio kusema refa huyo na FIFA walipata ahueni ya aina yake baada ya Mexico iliyotaewala mchezo ilipozawadiwa goli safi la siku, baada ya kipa wa Acmeroon kupangua mkwaju wa Dos Santos na kumwekea Peralta aliyetumbukiza ngoma kimiani
Matokeo hayo yanaifanya Mexico kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele pamoja na Brazil katjka kundi lao la A . Wababe hawa wawili (Mexico na Brazil) wanakutana siku ya Jumanne katika mji wa Fortaleza.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera akimpa maneno yake Refa kutoka Colombia Wilmar Roldan wakati wa mapumziko kwa kuwabania mabao mawili kipindi cha kwanza
Oribe Peralta akimchenga Samuel E'too kuifungia Mexico bao katika dakika ya 61 ya mchezo
Oribe Peralta akishangilia bao la Mexico dhidi ya Cameroon
Ni kweli lakini pia na Cameroun walinyimwa PENALTI ya wazi hivi hamkuona??
ReplyDelete