Hali ilivyokuwa katika mgomo huo abiria wakiwa wamejaa stand ya mabasi Kahama bila kujua hatma yao
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuzuia mgomo wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani ambao wanapinga kutozwa faini isiyo halali na kufanyiwa udhalilishaji na baadhi ya Askari wa kitengo hicho.
Mabasi yanayosafirisha Abiria Kutoka kahama kwenda mikoani leo yamegoma kusafirisha abiria wakishinikiza serikiali kuingilia kati suala la faini wanazotozwa na asikari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani.
farajimfinanga.com imefika eneo lakituo kikuu cha babasi mjini Kahama majira ya saa 12.30 asubuhi na kukuta mgomo huo ukiendela huku madereva wakiwa hawapo katika mabasi yao hali iliyosababisha kuwepo kwa msongamano.
 |
Kaimu mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga akiwa na maafisa wengine wa kikosi cha usalama barabarani pamoja na waandishi wa Habari
|
Kwa mujibu wa Madeleva ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai, wamekuwa wakipigwa faini na asikari wa mkoa wa Singida na huwalazimisha kulipa faini kubwa ya zaidi ya Shilingi 200,000 huku stakabadhi ikiandikwa shilingi 30,000 inayotambulika serikalini.
Wamesema pia wamekuwa wakilazimishwa kupigwa picha mbele ya mabasi yao wanapokamatwa hata kama wanaendesha mwendo mdogo na kwamba hubambikiziwa kesi, na kwamba baadhi ya madereva wamefikishwa mahakamani kwa kubambikiziwa makosa pale wanapogoma kutoa faini.
Aidha wanapinga kitendo cha ukatili alichofanyiwa dereva Mwenzao wa basi la Princess Munaa Lenye No. T 183 CRW ambaye alivunjwa mkono na askari wa kitengo hicho huko Mbezi Jini Dar es Salaam baada ya kugoma kunyang’anywa leseni yake.
Hata hivyo mgomo huo ulioanza saa kumi na mbili Asubuhi umedumu kwa takribani saa mbili na baadaye kuanza kwa safari, huku ikielezwa kwamba mgomo huo ulikuwa ni siri ya Madereva kwani Mawakala wanaokata tiketi hawakuwa na taarifa.
Akizungumza wakati wa mgomo huo Kaimu mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga aliwataka madereva kuendelea na safari zao kwani mgomo huo ni batili na wanaweza kuzisababishia kapuni zao hasara kubwa endapo ambiria watafungua Mashitaka mahakamani.
Amewataka madereva kufuata sheria za kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu zinazohusika ili masula yao yashughulikiwe pasipo kuleta athari yoyote.
Mgomo huo wa madreva wa mabasi umefanyika katika Miji ya Kahama, Bukoba, Mwanza, Msoma na Dar es Salaam huku taarifa zikisema licha ya mgomo huo kumalizika ila kwa sasa maderewa wanaendesha kwa mwendo wa chini kupita kiasi na kwa msongamano, hali inayozidi kuwachelewesha abiria.
|
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...