Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. 
Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata.. 
 Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, 
lakini  ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
Na anabainisha yote hayo katika wimbo wake mpya "Moyo wa mtu Kichaka" hapo chini. (Picha kwa hisani ya Vicky Kamata blog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2014

    Mhe. Vicky Kamata ametoa Ujumbe mzuri sana kwetu ni kuwa ''BINAADAMU HAAMINIKI''

    Unaweza kupanga na mtu mambo mengi kumbe mwenzako ana lake jambo moyoni isipokuwa utaelewa kila kitu kwenye matokeo yanayo fuata!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2014

    Kazi moyo Dada Vicky Kamata vijana tupo nawe. Duniani tunajua ibilisi wa mtu ni mtu pia. Mungu azidi kukuinua Dada mpendwa ubarikiwe ili adui waone baraka za Mungu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2014

    Dah wimbo na stori za huyu mdada zimenitoa chozi maana yalinikutaga kama hayo. Ila namsifu kwa kuweza kuibuka bila kuona noma wala nini. Life goes on.... Aliimba Celine Dion

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2014

    Dah wimbo na stori za huyu mdada zimenitoa chozi maana yalinikutaga kama hayo. Ila namsifu kwa kuweza kuibuka bila kuona noma wala nini. Life goes on.... Aliimba Celine Dion

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2014

    Wimbo ni mzuri na umetoa fundisho kwa watu mhh ila umenifanya nilie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...