Na John Nditi
WAREMBO 15 wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania kunyakua taji la Miss Morogoro 2014 litakalofanyika leo Juni 13, kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera ya Mjini Morogoro.
Katika kinyang’anyiro hicho, Msanii wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’ anatarajia kupanda jukwaani kutoa burdani wakati wa kumsaka malikia wa Redd’s Miss Morogoro wa mwaka huu.
Warembo hao wamejitokeza kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Msomi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) , Diana Laizer aliyelitwaa mwaka 2013 kwenye ukumbi huo huo baada ya kuwashinda wenzake 9 waliokuwa wameshiriki.
Mratibu wa shindano hilo, Frank Kikambako pamoja na Mwalimu shindano hilo, Salvina Kibona, kwa nyakati tofauti mbali na kumtaja Msanii Tundaman, pia wasanii wengine watashiriki kunogesha wakati huo .
Mwalimu wa warembo hao anasema kuwa mwaka huu washiriki wamejitokeza wengi zaidi kutokana na kutambua umuhimu wa shindano hilo ndani ya jamii na kwamba wote wanazo sifa na vigezo vinavyolingana katika kuwania taji hilo.
Aliwataja warembo hao kuwa ni , Lucy Diyu. Alexia Shayo, Mwasuma Ibrahim , Angle Shio, Sia Mtui, Bossa Emmanuel, Neema Nachenga, Prisca Mengi, Welo Eliude, Hawa Mshana, Lissa Mdolo, Magreth David na mwingine aliyemtaja kwa jina moja tu la Caren.
“ Tunao warembo wenye sifa zinazofanana ...na hii italeta ushindani mkali wa nani anaibuka kuwa malkia wa Redd’s Miss Morogoro kwa mwaka huu” alisema Mwalimu wa Warembo hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...