Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne) nje ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe 12.6.2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa wamebeba mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...