Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Eng. Stella Manyanya akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi huduma
ya Option B Plus Mkoani Rukwa jana tarehe 07 Juni, 2014 katika Kijiji
cha Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Huduma hiyo ina lengo la kutoa tiba
ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito
kwenda kwa mtoto mchanga. Kaulimbiu ya huduma hiyo ikiwa "Amka Sasa
Tokomeza VVU kwa Watoto, Kama mjamzito Pima VVU kwa maisha Bora, Tiba
inapatikana"
Mkuu
wa Wilaya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (kulia) akipokea taarifa ya
utaratibu maalum na tiba ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga kutoka kwa wataalamu wa tiba
alipotembelea banda la Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa muda
mfupi kabla ya uzunduzi wa huduma hiyo katika viwanja vya Tamasenga
Wilayani Sumbawanga. Katika salam zake Mkuu huyo wa Wilaya amewataka
wahudumu wa afya kuzingatia viapo vyao kwa kutunza siri za wagonjwa
hususani walipomwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akisoma risala kwa Mgeni Rasmi
katika hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma ya Option B Plus. Katika risala
yake amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoani Rukwa yameongezeka
ambapo sasa yapo kwa kiwango cha asilimia 6.2. Alisema mpaka sasa jumla
ya watumishi 225 sawa na asilimia 75% wameshapatiwa mafunzo ya utoaji wa
huduma hiyo ambapo matarajio ni kufikia watumishi 302. Alieleza kuwa
mpaka sasa jumla ya vituo 116 vinatoa huduma hiyo sawa na asilimia 83%
lengo likiwa kufikia vituo 139 hadi kufikia mwezi Septemba 2014.
Hafla
hiyo ya uzinduzi ilipambwa na maandamano ya awali yaliyokuwa yakitoa
ujumbe wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito
kwenda kwa mtoto mchanga.
Meza
kuu ikipokea maandamano hayo kwa kupiga makofi. Wakwanza kushoto ni
Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Ndugu Erasmus Rugarabamu, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta na Mganga
Mkuu Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha kushoto akiteta jambo na
Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Rukwa Dkt. Hansi Ulaya muda mfupi kabla ya
uzinduzi wa huduma hiyo.
Baadhi ya wadau wa huduma ya afya waliohidhuria katika hafla hiyo.
- Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...