Mtoto Maimuna Yahaya akiwa
na Mama yake Mzazi Tunu Juma.
Msaada unahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Mtoto Maimuna Yahaya (11)
anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Irente
Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili. Yeye anasumbuliwa na tatizo la mifupa
na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu
wa viungo na mtindio wa Ubongo.
Mama wa mtoto
huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna
katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea
kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.
Bi. Tunu
amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya
siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma
Maziku anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa
kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa
wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu. Mahali
wanapopatikana: Lushoto Mabwawani
Mawasiliano:
Namba ya simu ya mama mzazi:+255712504768 Namba
ya Tigo Pesa imesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na
Namba ya Airtel Money ni 0787204160 imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...