Kikosi cha Mucoba Fc kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa fainali na Mbaspo Academy na kufanikiwa kunyakua kikombe cha Muungano katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Igowole. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo akimkabidhi kikombe cha ubingwa nahodha wa timu ya Mucoba Fc Emanuel Sabinus baada ya kuwafunga Mbaspo academy kwa mikwaju ya penati 7-5 katika mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi Igowole wilayani Mufindi.
 Nahodha wa timu ya Mucoba Fc Emanuel Sabinus akinyanyua juu kombe la ubingwa wa Muungano Cup mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo.
=======  ===== =======
Na Denis Mlowe,Mufindi

FAINALI za 18 za mashindano ya kugombea kombe la Muungano  zilimalizika juzi kwa timu ya Mucoba Fc ya wilayani Mufindi mkoani Iringa kunyakua taji hilo kwa kuwafunga mabingwa watetetezi Mbaspo Academy ya mkoani Mbeya kwa mikwaju ya penati 7-5 katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Igowole Mafinga.
 
Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo alishuhudia kila timu ilianza kwa kumsoma mpinzani wake kutokana na kujuana walikuwa Mucoba Fc walioanza kutawala katika dakika ishirini za mwanzo na kumweka katika wakati mgumu golikipa wa Mbaspo kwa mashuti ya kushtukiza, kosa kosa ziliandelea hivyo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa kusomana kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza na ndipo katika dk ya 70 mshambuliaji hatari wa Mucoba Fc David Mhanga aliwapatia goli timu yake baada ya ushirikiano mzuri na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Hussein na dk ya 75 David Mhanga aliongeza goli la pili kwa upande wa Mucoba FC.
 
Baada ya goli hizo mbili Mbaspo walikuja juu na ndipo katika dk ya 84 mchezaji aliyewateka mashabiki wa soka kwa kiwango chake Soud Mlindwa aliipatia bao timu yake na zikiwa zimesalia sekunde chache kumalizika kwa mpira na baadhi ya wachezaji wa Mucoba kuanza kushangilia ushindi Thabit Juma katika dk. 90 alisawazisha goli ndipo hatua ya kupigiana penati alipochukua hatamu.
 
 Timu ya Mbaspo waliweza kupata penati zao kwa kupitia Eliah Jimmy, Mpoki Mwansansu, Masoud Yusuph, Soud Mlindwa na Boaz Patson  waliokosa ni Thabit Juma na Michael Masinga.
  
Kwa upande wa Mucoba waliofunga penati zao ni Benjamin Mlowe, Ima Mwakajinga, Stanley Mwazangila, Elisha Mwasieni, Denis Lameck na Daud Mwanga aliyekosa ni Reward Abraham na katika mikwaju hiyo shujaa wa timu ya Mucoba alikuwa golikipa wake aliyeweza kupangua penati mbili.
 
Mara baada ya kumalizaka kwa mchezo huo Tanzania Daima lilizungumza kocha wa timu ya Mbaspo Academy Maka Mwarusye, aliwapongeza Mucoba kwa kuchukua ubingwa na kuahidi kwenda kujipanga upya kwa msimu ujao wa mashindano na kwa upande wa mchezo  ulikuwa mzuri kwa upande wa timu zote ila katika mchezo wa soka  kuna kushindwa na kushinda ua sare, hivyo hatua ya penati ni bahati nawapongeza mabingwa.
 
“Mashindano yalikuwa mazuri ingawa kulikuwa na changamoto zake na changamoto hizo ni viwanja kutokuwa na ubora na kuboresha waamuzi itasaidia sana nawapongeza sana Mucoba na vijana wangu kwa kufika fainali kwa mara ya pili” alisema Mwarusye.
 
Bingwa wa mashindano hayo timu ya Mucoba alijinyakulia shilingi milioni 3 na kombe lenye thamani ya shilingi milioni 1.2 na medali za dhahabu, mshindi wa pili timu ya Mbeya City iliondoka na kitita cha shilingi milioni 1.5.
 
Zawadi nyingine zilikwenda kwa mwamuzi bora wa mashindano hayo ambao Steven Makuka, Hashim Mgimba na Erasto Msalilwa waliojipatia sh. Elfu 50 kila mmoja, mchezaji bora wa mashindano hayo  golikipa wa Igowole Fc sh. Laki 2, Mfungaji bora Shadrack Tamimu sh. Laki 2 wa Mbeya City na timu yenye nidhamu Mbeya City sh. Laki 5 na kombe.
 
Mashindano ya Muungano yanayofanyika kila mwaka katika wilaya ya Mufindi na kuratibiwa na Daud Yasini yalidhaminiwa na  Chai Bora ,Asasi Limited, benki ya Mucoba ,na  PPF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...