Afisa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania mkoani Mwanza Liston Chale (kulia), Meneja Matukio, TBL Mwanza Eric Mwayela, na Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo wakimkabidhi Kapteni wa timu ya Musoma Veterani, Ramadhani Magoe (kushoto) kombe baada ya kutawazwa mabingwa wa fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa jana baada ya timu yake kuwafunga Milango Kumi FC ya Kahama mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana. Mabingwa hao wataiwakilisha Kanda ya Ziwa kwenye fainali za taifa.
Wachezaji wa Timu ya Musoma Veterani, wakishangilia na kombe lao walolipata baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Milango Kumi FC ya Kahama magoli 3-2 na kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...