Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyika Kibara, mkoani Mara. Pia semina hiyo ilishirikisha viongozi wa vijiji, vyama pamoja na madiwani lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa sheria na kanuni za uchimbaji wa madini. Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mhe. Kangi Lugora. Kushoto ni Kamishna Msaidizi – Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Mhandisi Fredy Mahobe.
Mtalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sekretarieti ya maandalizi ya semina hiyo ikiwajibika.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (hayupo pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...