Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Kimara Baruti kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mbele ya ofisi za TRA Kimara Baruti ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa tatizo kuwabwa la foleni linadhoofisha uchumi hivyo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi mara moja,pia alisema atazungumza na viongozi wa ngazi za juu wa CCM kuwapa kipaumbele wakazi wa Ubungo na Kawe waweze kupata maji mwanzoni katika miradi ya maji inayokuja.
Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye alipohutubia wakazi wa Kimara Baruti leo.
Hamida Issa Selemani akielezea umati wa wakazi wa Kimara uamuzi wake wa kujiunga na CCM baada ya kuchoshwa na siasa chafu za chama cha CUF.Hamida alishakuwa Diwani na Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Biharamulo na mgombea Ubunge wa CUF jimbo la Biharamulo Magharibi
Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo akimpa mkono Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kutangaza kujiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo pamoja na Hamida Issa Selemani na wanachama wengine zaidi ya 420 wakila kiapo cha kuwa wanachama watiifu wa CCM Jumuiya ya Wazazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...