Madereva wa Mabasi yanayokwenda katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Kagera jioni hii wameingia kwenye mgomo wa kutosafirisha abiria wakiwa mkoani Singida, kwa madai kwamba wanatozwa faini kubwa sana na Askari wa Usalama barabarani mkoani hapo.Baadhi ya abiria wanaosafiri na mabasi hayo wameulalamikia uamuzi wa madereva hao, kwani ni kama wanapewa adabu kwa uamuzi huo.Globu ya jamii inaendelea kufatilia sakata hilo kwa ukaribu zaidi na tutaendelea kufahamishana zaidi.

Kama faini ni kubwa,kwa ajili ya kudhibiti usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara, sioni sababu za mgomo huu.
ReplyDeleteLakini kama kuna mengine, inabidi wahusika washughulikie suara hili.