Na Mwene Said 

MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha (pichani wakiwa, amefikishwa katika Maha kwenye shughuli zao siku za nyuma) kama ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
 Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2014

    Ndio shida ya kushindana na Mwanamke. Mwanamke akikushinda bora kumkimbia. Ukishindana naye Kama unashindana na mwanamume mwenzio haya ndio matokeo yake!

    ReplyDelete
  2. Aisee kama tamthilya vile

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2014

    Dah!Mie siamini kabisa, bongo yetu kwa kuoneshana ndio penyewe. Somebody here wants to make a statement!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2014


    Wengi wetu tutaleta ule ujinga wetu - kwamba...... "baba kambaka bintiye mtoto basi mama anahimizwa au anaona bora tuyamalize nyumbani maana baba akienda jela tutakula wapi?"

    Jamaa lazima ajibu tuhuma, kama hana hatia basi itaamuliwa na jaji.

    Haya anzeni na hili zongo. mdau Alexbura Dar.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2014

    sheria ni msumeno. tusubiri

    ReplyDelete
  6. Duuuhh!!! Tatizo ni kubwa mno na halina mshindi. Pande zote maisha hayatakuwa kama ilivyokuwa zamani hata kama mwisho wake utakuwa vizuri kwa upande huu wala huo.
    Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2014

    ..
    Ninakubaliana na Mhoja hapo juu... Life will never be the same again...sadly!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...