Na Mwandishi Wetu
Shirika la Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), linaendesha kambi za
upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Lengo la kambi hizi ni
kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama
wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga
tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha
ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi ambalo lilianzia mkoa
wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 ambao watu waliopima VVU ni 1380, linaendelea mkoa wa Shinyanga ,
Wilaya ya Kahama, kwenye Viwanja vya Barcelona,
kuanzia tarehe 04/06/2014,
kwa siku mbili mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni. Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika Mkoa wa Geita na Mkoa wa Kagera.
kwa siku mbili mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni. Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika Mkoa wa Geita na Mkoa wa Kagera.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma
mbalimbali zitatolewa kwenye kambi hizi zikiwemo;
·
Upimaji wa Shinikizo la damu
·
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
·
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa
Unene)
·
Utoaji wa dawa za Minyoo
·
Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na
Matatizo
·
Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
·
Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji
wa Afya.
Huduma zote hizi
zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na
kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI
Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji
wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa
Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme
ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia
nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja
na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa kanda ya ziwa
wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri
wa afya zao Bure.
NSSF
INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Lucy Simbila akizungumza kabla hajamkaribisha Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga afungue Kambi ya Upimaji Afya.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dk. Charles Rweikiza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Wilaya ya Kahama. Kushoto ni Dk.Mzige, wa tatu kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF Kahama , Salum Salahange, Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk.Lucy Simbila na Ofisa Uhusiano NSSF, Jumanne Mbepo.
Dk.Mzige Akitoa Ushauri kwa mmoja wa wakazi wa Kahama aliyejitokeza kupima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...