Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa |
Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imekamilisha rasimu ya miswada mitatu
ya sheria za usalama wa mtandao ili kudhibiti uhalifu katika mitandao nchini
Tanzania.
Akiwasilisha
makadirio ya bajeti ya wizara hiyo, Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
Profesa Makame Mbarawa alitaja miswada hiyo kuwa ni sheria ya usalama wa
mtandao, sheria ya kulinda taarifa binafsi, sheria ya miamala ya kielektoniki
na shaeia ya kudhibiti uhalifu mtandao na kompyuta.
Alisema
rasimu hizo zimewasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili ziweze
kuandaliwa kwa mujibu wa taratibu za uandishi wa sheria.
Pia
alisema wizara hiyo imetengeneza kanuni mpya zinazosimamia mawasiliano kupitia
mitandao ya simu ambayo ilianza kazi mwezi oktoba mwaka mwaka jana kwa
makampuni ya nje kutakiwa kulipa senti 25 za marekani kwa kila dakika moja ya
mazungumzo ya simu zinazongia nchini kutoka nje.
Profesa
Makame aliongeza kuwa katika kanuni hiyo
mpya imeweka mgawanyo wa mapato hayo ya senti 25 ambapo serikali kupitia hazina
inapata senti saba, watoa huduma wanapata senti kumi na tatu na senti tano ni
kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ikiwa ni pamoja na kumlipa mwekezaji wa
mtambo huo.
Wakati huo huo, mtaalamu wa TEKNOHAMA upande wa usalama wa mtanda Bw. Yusuph Kileo anabainisha kwa kuwa sheria mtandao zinatofautiana sana na sheria nyingine, mapitio yake yanapaswa kufanyika mara kwa mara
kutokana na sababu za msingi za makosa mtandao kubadilika badilika kutokana na
ukuaji wa haraka wa teknoljia hivi sasa.
Bw. Kileo anasema uhalifu
mtandao umeendelea kukua kwa kasi katika maeneo mbali mbali duniani. Hii
imepelekea Microfoft kuanzisha kitengo maalumu kitakacho ongeza uwezo wa
kukabiliana na usalama mtandao kama inavyosomeka kwenye taarifa hii “HAPA”.
Wakati
huo huo takwimu zilizo tolewa na Idara ya upelelezi kupitia kitengo cha
kukabiliana na uhalifu mtandao ya nchini Sirilanka zimeonyesha ukuaji wa makosa
hayo katika nchi hiyo yameendelea kukukua kwa kasi. Takwimu hizo zinapatikana
katika tovuti yao na kusmeka “HAPA”.
"Pamoja
na nguvu kubwa ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao bado changamoto kubwa hasa
katika nchi za afrika imekua ni upungufu wa sharia zinazoweza kuwafanya
wahalifu kuchukuliwa hatua stahiki pale inapothibitika uhalifu mtandao
kufanyika.
"Nchi
mbali mbali zimeendelea kuboresha sharia zao na kuzifanya kua kali zaidi ili
kuweza kuhimili vishindo vya wahalifu mtandao ambapo wanaonekana kushika kasi
ya kipekee. Moja ya nchi hizo ni hapa kwetu TANZANIA", anamalizia Bw. Kileo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...