MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando ameibuka na wimbo mpya uitwao Facebook. 

Akizungumzia  wimbo huo, Rose amesema  ana imani wimbo huo utakuwa kivutio kikubwa kwa jamii hasa vijana kwa sababu una ujumbe mzuri ambao utagusa wengi.

“Sitaki kuwaambia nimeimba nini, lakini Facebook ni wimbo mzuri na mashabiki wangu naamini wanatambua kwamba mimi si mtu wa masihara ninapotunga kazi zangu,” alitamba mwimbaji huyo.

Alieleza kuwa wimbo huo utakuwa katika albamu yake mpya iitwayo Kamata Pindo la Yesu anayotarajia kuizindua jijini Dar es Salaam katika siku itakayotangazwa wakati wowote kuanzia leo.Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu msanii huyo ni pamoja na Mteule Uwe Macho, Nipe Uvumilivu, Yesu Nakupenda, Akina Mama, Nakuuliza Shetani, Yerusalemu, Mwambieni Mungu na Nakaza Mwendo.

Pia nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni Kitimutimu, Imani, Onjeni, Sikilizeni Enyi Makahaba, Mungu Wangu, Moyo Wangu, Najitoa Sasa, Hey Mbona Watenda Dhambi na Wapendwa.

Nyingine ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Nyimbo hizo zipo katika albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa na Utamu wa Yesu.

Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...