Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea
msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha Ngumi za
Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel
Bw. Pratap Ghose.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na
viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono kwa pamoja
kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi Milioni kumi kama
msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi Tanzania (BFT).
Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani
kwa Zantel baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa
ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na kulia ni
Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George Voniatis.
Picha na Genofeva Matemu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...