Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya ya Ujenzi wa Nyumba 5,000 za gharama nafuu.
Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo mchana katika Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Mhe.Prof Mark Mwandosya, ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe Mashariki, na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Mhe.Aggrey Mwanri.
Pichani wanaosaini kuanzia kulia ni kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi,Bw.Meckson Mwakipunga (M/Kiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya na Bw. Said Mderu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi akibadilishana Mkataba na M/Kiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga baada ya kutiliana saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga akielezea kuhusu Mradi mzima, baada ya kutiliana saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Mhe.Prof Mark Mwandosya. Waziri ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe Mashariki akitoa shukurani baada ya mkataba wa Ujenzi wa Nyumba 5,000 za gharama nafuu kusainiwa.
Baadhi ya Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakifuatilia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa nyumba 5,000 za gharama nafuu katika Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati
Gharama nafuu ni kiasi gani na nymba ya ukubwa gani??!
ReplyDelete