Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana. 
 Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua ndani ya Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
 Pichani baadhi ya Screen zikionyesha picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC lililopatikana kwa msaada wa Serikali ya China.
 : Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana mara baada ya gari hilo kukabidhiwa na kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2014

    this is why I like Chinese government. hawatoi pesa sababu wanajua italiwa na wenye matumbo. huwa wanafanya kweli na ndio maana nchi inapiga hatua.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2014

    jamani wachina ni marafiki wetu. hiyo haina shaka. lakini ingekuwa vyema tuwaombe vitu viwili ama vitatu vikubwa basi. sasa hata gari la utangazaji kusaidiwa kwa kweli ni masikitiko makubwa. hawa tungewaomba watujengee bandari, reli ya kati kwa kiwango cha umeme, na gasi ama mradi mkubwa wa umeme. haya ni mambo yangepanua uchumi wa nchi yetu ambao ungetuwezesha hata kunjinunulia magari kama hayo mengi!! hivi sisi tukoje? hatuoni wanachofanya wenzetu kenya? mhe rais amejitahidi sana sioni kama sisi wengine tunamsaidia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...