Liberatus "Libe"
 mgombea nafasi ya Urais

Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliye weza kufika kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara jana Meadowbroak Park. Pia tunapenda kuwashukuru wale walio kuwa na nia ya kuja lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao wakashindwa kutimiza hadhma hiyo.  Asanteni!

Pia, Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kuwashukuru wagombea wengine kwa kujitokeza na kuonyesha ushirikiano chanya na kufurahia mazungumzo na wapiga kura; asante mama Salma Manyoka/mgombea makamu wa Rais, asante Heriet Shangarai/ mgombea makamu wa Rais, asante Solomon Cris/mgombea makamu wa katibu
 
Mama Salma/Mgombea makamu wa Rais
Zaidi, shukrani zetu za dhati zinaenda kwa Ndg. Hamza Mwamoyo/Mwenyekiti wa board, Mzee Safari/ Mkiti wa tume ya uchaguzi na mke wake mama Safari, kaka yetu Jabil  Jongo/ mjumbe tume ya uchaguzi na mchungaji Malekela kwa kuonyesha mapenzi yasio na ukomo kwa jumuia yetu ya DMV.
 
Heried Shangarai/Mgombea makamu wa Rais
Mwisho, tunawashukuru wana DMV wote kwa kuwa na ushirikiano thabiti na kusaidiana kwenye raha na shida. Kama imani ya kimsingi ya “, Team Libe for DMV Community President 2014”inavyo sema “binadamu tupo hapa ili tushirikiane na sio kushindana wala kutengana.”
Solomon Cris/Mgombea makamu wa katibu

Team Libe for DMV Community President 2014 
wishes all Muslims Ramadan Kareem.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...