Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad Wilson  Ngewe  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014. 

Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...