KARIA KUFUNGUA KOZI YA MAKOCHA LEO
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (pichani) atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kozi ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Uzinduzi wa kozi hiyo ya wiki mbili utafanywa leo (Juni 10 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Makocha zaidi ya 20 wenye Leseni C kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika kozi hiyo inayoendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni. Mkufunzi mwingine wa kozi hiyo anayetambuliwa na CAF ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI

Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
.jpg)
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...