Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika
kuwataarifu wananchi na wateja wake wa huduma
ya treni ya Jiji kuwa hiyo imesitishwa
kwa muda wa siku 3 kuanzia kesho Juni 19, 2014 hadi Jumammosi Juni 21, 2014. Aidha huduma hiyo
itaanza tena hapo Jumatatu Juni 23, 2014 kwa kufuata ratiba yake ya kawaida.
Uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi
ikiwemo kufanyiwa matengenezo vichwa vyote vya viwili ambavyo vimekuwa vikihudumia treni hiyo
ya Jiji. Vichwa hivyo vinapaswa kufanyiwa ukarabati katika Karakana Kuu ya TRL
Morogoro na kwamba vitarejeshwa Jijini Jumapili Juni 22, 2014.
Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na
wateja wake wote jijini kwa usumbufu utakaojitokeza.
-Tamati-
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Juni 18, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...