Taasisi ya Faridas foundation inatarajia
kufanya uzinduzi wake rasmi siku ya tar 28/6/2014 siku ya jumamosi
katika ukumbi wa crystal hall, blue pearl hotel, ubungo plaza kuanzia
saa 6 hadi 12 jioni.
Katika siku hyo taasisi itatoa misaada mbali mbali kwa
walemavu ikiwemo baiskeli za walemavu, vyerehani, vifaa vya shule na
vifaa vingine muhimu kwa walemavu ukiwa kama mdau au mtanzania
unayeguswa na walemavu na ungependa kuhudhuria siku hyo maalumu kadi
zinapatikana kwa mchango wa shilingi laki moja na kuendelea hii
ikiambatana na chakula cha mchana vinywaji na burudani mbalimbali pia
utakuwa umesaidia kuongeza idadi ya vifaa vitakavyotelewa kwa walemavu
mbali mbali. Kutoa ni moyo sio utajiri.
Endapo una kampuni au ungependa
kushiriki kama kampuni au taasisi kwa kudhamini pia nafasi bado zipo
wazi wasiliana nasi kupitia +255715186262 au email
faridasfoundation@gmail.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...