Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na  Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaoendelea Jijini London, Uingereza. 
Kwenye sherehe za ufunguzi, waandaaji wa mkutano huo walisifia nchi zinazochangia kuleta amani kwenye maeneo yenye migogoro duniani . Aidha walisifu hatua ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kukubali na kusaini Tamko la Umoja wa Mataifa la Kukomesha udhalilishaji wa Kijinsia katika maeneo yenye migogoro. (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).  
Mwandaaji wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro, Mhe. William Hague, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza 

 Mwandaaji mwenza ambaye ni mcheza filamu nyota  Bi. Angelina Jolie, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Wakimbizi, akitoa hotuba yake ya  ufunguzi kwenye mkutano huo unaoendelea Jijini London, Uingereza.
 Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiweka saini hati ya tamko la jumla la mkutano huo  likiwataka washiriki kuchukua hatua sasa ya  kukomesha udhalilishaji wa kijinsia kwenye maeneo yenye migogoro.
Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaondelea Jijini London, Uingereza. kuanzia tarehe 11 hadi 13 Juni, 2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...