Mwenyekiti wa Kundi la Afrika Nagmeldeen Elhassan kutoka Sudan akizungumza wakati wa mkutano wa kundi la Afrika uliokuwa ukitoa taarifa kwa ufupi kwa mawaziri wa mazingira Afrika.kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Balozi Ahmed Swaraldhab kutoka Wizara ya Mambo ya Nje nchini Sudan. Waziri Samia anahudhulia Mkutano huo kwa kumuwakilisha Waziri wa Mazingira Tanzania ambae ni mwenyekiti wa Mawaziri wa Mazingira Afrika.
Maafisa kutoka katika serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki katika mkutano wa kundi la Afrika kwenye mkutano wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini Bonn Ujerumani Leo.
Waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa rais Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia Nchi Bw. Richard Muyungi katika mkutano wa kundi la G77 na China, kwenye mkutano wa Mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bonn Ujerumani..
(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...