MAREHEMU REDEMPTA 
KATONDAABELA (MAMA RWEKAZA)

Familia ya Prosper Mutafurwa wa Mtaa wa Mwale, Tandika Maguruwe, Dar es salaam. Inasikitika kutangaza kifo cha Mke wake mpendwa Redempta KatondaAbela ai Mama Rwekaza (Pichani) kilichotokea alfajiri ya Jumapili tarehe 01/06/2014 akiwa usingizini.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote walipo.
Mipango ya mazishi inafanyikia Nyumbani kwa Mume wa marehemu Tandika Dar es salaam.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 04/06/2014 kwenda Katoke, Buyango, Kiziba, Bukoba na mazishi yatafanyika Siku ya Ijumaa tarehe 06/06/2014 huko huko Katoke,Buyango, kiziba, Bukoba.
Glob ya Jamii  inatoa  pole kwa 
familia nzima, ndugu, jamaa na marafiki wote

BWANA AMETOA NA BWANA 
AMETWAAJINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2014

    Pole Bwana Polo kwa msiba huu mkubwa.

    ReplyDelete
  2. RIP mama Rwekaza, tutakukumbuka daima. Ni majonzi makubwa. Pole mjomba & family, Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2014

    Nimepokea taarifa za msiba wa Mama Lwekaza kwa mshituko mkubwa,daima tutakukumbuka kwa ucheshi wako pamoja na busara zako,bwana alitoa na bwana ametwaa jinalake liimidiwe, natoa pole kwa mjomba Prosper Mutafurwa pamoja na familia nzima ya Mutafurwa,mwenyezi mungu awatia nguvu katika kipindi hiki kigumu cha msiba, from Thadeo Mpelasoka - songea

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2014

    Nimepokea taarifa za msiba wa mama Rwekaza kwa mshituko mkubwa,daima tutakukumbuka kwa ucheshi wako pamoja na busara zako,bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe, natoa pole kwa mjomba Prosper Mutafurwa pamoja na familia nzima ya Mutafurwa kwa ujumla,mwenyezi mungu awatia nguvu hasa katika kipindi hiki kigumu cha msiba, from Thadeo Mpelasoka - songea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...