Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF- Ladislaus Mwamanga amewataka watumishi wa Mfuko huo kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kufanya kazi ili mpango wa kunusuru kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na serikali.

Mwamanga ametoa kauli hiyo mkoani Mtwara wakati akifungua warsha elekezi ya siku mbili kwa maafisa ushauri, ufuatiliaji, wahasibu  na waratibu wa mikoa na wilaya ikiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa mradi wa TASAF awamu ya tatu katika halmashauri 22 ambazo zimeanza utekelezaji wa mpango huo.

Halikadhalika Mwamanga amewataka kushirikiana, kuwa makini  na kutokiuka taratibu na matumizi ya fedha za mpango huo na kufuata miongozo sahihi ya kazi kwa sababu serikali imeona njia pekee ya kuwakomboa watu waliosahaulika ni kuwaingiza katika mpango.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati waliokaa) na wakurugenzi wengine wa TASAF Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waratibu wa mikoa wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili mjini Mtwara
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akifungua Warsha elekezi  ya siku mbili kwa maafisa ushauri na ufuatiliaji, waratibu wa mikoa, waratibu na wahasibu wa mamlaka ya eneo la utekelezaji wa halamashauri 22 nchini inayofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha SAUT Mjini Mtwara
 Mkurugenzi wa mpango wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akitoa maelezo juu ya mpango wa kuzinusuru kaya masikini na zilizo katika mazingira hatarishi katika warsha hiyo
 Washiriki wa warsha hiyo wakiwa wamenyoosha mikono juu kama ishara ya kukubaliana na jambo wakati Mkurugenzi mkuu wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo
 Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada ilyokuwa ikiwasilishwa. 
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa makini uwasilishi wa moja kati ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, na wakurugenzi wengine toka TASAF Makao Makuu wakiwa kwenye picha ya pamoja  na waratibuwa  mamlaka ya eneo la utekelezaji wa Halamashauri 22 nchini (waliyosimama) Mjini Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...