100.5 Times Fm Radio imetoa kiasi cha shilingi milioni tatu kwa albino wa wilaya ya Temeke, Dar es
Salaam kama sehemu ya mchango wao kwa jamii hiyo yenye ulemavu wa ngozi inayokumbwa na
changamoto nyingi.
Katibu wa Kampuni ya Times Fm Radio, Amani Joachim ameukabidhi uongozi wa chama hicho hundi
halisi akiwa ameambatana na Aluta Warioba (Meneja Vipindi Msaidizi) na Mzee Chapuo kutoka
katika idara ya ubunifu.
Amani Joachim aliwaomba wapokee kiasi hicho kwa kuwa bado Times Fm itaendelea kushirikiana
nao katika kupambana na changamoto zinazowakabili na kuhamasisha jamii kuendelea kuonesha
upendo kwa walemavu.
Baada ya kupokea hundi halisi ya kiasi hicho cha fedha, mwenyekiti wa chama cha Albino Temeke,
Khasim Kibwe alitoa shukurani zake kwa chombo hicho cha radio na kueleza kuwa fedha hizo
zitasaidia sana katika kununua mafuta maalum ya ngozi kwa wanachama wake.
“Kwanza nafurahi sana kwa kutujali sisi Albino. Lakini vilevile wito kwa jamii nao waige mfano huu
wa 100.5 Times Fm nao waweze kuwachangia watu wenye albinism. Baada ya kuwa kiongozi,
nakumbuka hata mlipotushirikisha katika mpira mwaka 2008 tuliona urafiki wenu wa karibu,
vilevile sasa tunauona urafiki wenu umekamilika zaidi. Ni watu ambao mnajali watu wenye mahitaji
maalum.
“Jamii iendelee kusikiliza Times Fm na wale wenye mahitaji wengine basi waipende Times kwa kuwa
inapenda watu wa aina zote.” Amesema bwana Kibwe.
Viongozi wengine wa chama hicho waliokuwepo ni pamoja na muweka hazina, Said Ndonge na
katibu wa chama, Gaston Mcheka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...