Ankal akiwa na Mdau Maggid Mjengwa.

Ndugu zangu, 

Septemba kumi, 2006 nilikutana na ndugu na kaka yangu Muhidin Issa Michuzi pale Food World Restaurant, Maktaba Street, Dar es Salaam.

Kaka Michuzi na mimi tulizungumza kwa kirefu juu ya masuala ya kublogu. Wakati huo blogu ilikuwa ni kitu kipya sana hapa nyumbani. Na hakika hapa nyumbani alianza Muhidin Michuzi kuwa na blogu ya habari na picha. Mimi ni kati ya wachache tuliofuatia kwa hapa nyumbani.

Kwenye mazungumzo yetu pale Food World, nilimwambia Michuzi niwe nachangia kwenye Michuzi blog kwa kumtumia picha na habari kutoka vijijini, ni kwa vile nimekuwa nikiishi Iringa na kufanya kazi za vijijini tangu 2004. 

Michuzi aliniangalia na kusema; " Maggid, mimi nafikiri nawe uwe na blogu yako mwenyewe yenye kutoa zaidi taswira za maisha ya vijijini".

Michuzi na mimi tumefahamiana tangu miaka ya 80 mwishoni. Kilichotuunganisha na Michuzi tangu wakati huo ni picha, kama Michuzi, nami pia nimekuwa na mapenzi makubwa na picha tangu utotoni.

Michuzi aliufahamu uwezo wangu, na ndio maana akaona bora niongeze nguvu kwa kuanzisha blogu yangu mwenyewe.

Na ndipo hapo ' Mjengwablog' kama wazo l a ' blogu kama kijiji' likazaliwa, na Jumanne ya Septemba 19, 2006, ndipo picha ya kwanza na maelezo iliingizwa kwenye Mjengwablog. Naam, nimeratibu shughuli za ' Mjengwablog' kama ' Kijiji' tangu 2006. Ndio sababu ya kuitwa ' Mwenyekiti'. Ina maana ya ' Mwenyekiti' wa Kijiji cha ' Mjengwablog'!

Na profile picture yangu ya kwanza kwenye Mjengwablog ilikuwa nimetinga shati hilo hilo nililovaa nikiwa na Michuzi ( Pichani).

Hakika, nyingine ni kumbukumbu muhimu sana katika kuandika historia ya chimbuko la blogu Tanzania. Kuna umuhimu wa kuweka kumbukumbu hizi katika maandishi ili yasaidie vizazi vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2014

    Kweli Ankali Michuzi wewe ni Sheikh na Shariff sana!

    Sasa wajameni wale wanaodai Michuzi anawabania kivipi kama tunavyoona hayo maelezo hapa yeye Michuzi alibariki na kutoa mwongozo ili na nduguye Mjengwa aanzishe Boglu yake?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2014

    Duhh kweli Michuzi una moyo safi kama Kiongozi wetu Mkuu Jakaya Kiwkete!

    Kwa hulka zetu na roho mbaya sio jambo rahisi kwa uamuzi alioutoa Michuzi hapo.

    Kwa kweli kazi zenu wote Mjengwa na Michuzi zitapata baraka kwa kuwa mna nia njema!

    Yaani umempa Mjengwa mchongo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2014

    Mbarikiwe kwa kazi zenu,

    Kwa wengi wetu kwa roho zetu mbaya isingekuwa rahisi mtu umpatie mwenzako mchongo kama huo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2014

    Hongera saana kaka zangu wote wawili juhudi ya kazi zenu zimesaidia kiasi kikubwa kwa kutuelimisha na kujenga jamii yetu ya watanzania.

    Mikidadi-Denmaark

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2014

    Kubana kwa michuzi kupo ktk maoni tu yatolewayo hapa hasa yenye mlengo wa kushoto......yenye kurekebisha wanaotuyumbisha na kutusababishia ugumu kadri siku ziendavyo....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...