Na
Sultani Kipingo
Wakiwa
wameshinda mara mbili katika michezo yao ya kwanza ya Kombe la Dunia 2014,
Costa Rica wamedaka tiketi ya kwenda katika raundi ya mtoano ya 16 huku Brazil.
Baada
ya kufanya maajabu kwa kuifunga Uruguay katika mchezo wao wa fungua dimba,
Costa Rica wamaeitungua Italy 1-0 leo katika mchezo mkali wa kundi D katima
uwanja wa Pernambuco mjini Recife.
Goli lao la ushindi limepatikana
dakika chache kabla ya mapumziko pale kiungo wao mahiri Bryan Ruiz alipotia
ndinga kimiani kwa kichwa kufuatia majalo tamu ya kona ya Junior Diaz.
Mpira huo baada ya kupigwa kichwa
na Ruiz uligonga besela na kudunda ndani ya goli. Teknolojia mpya ya kugundua
magoli ilithibitisha hilo ni bao kwani mpira ulishavuka mstari. Matokeo hayo yanaihakikishia Costa Rica nafasi
katika raundi ya 16 bora na hapo hapo wanakuwa wameifungashia virago Uingereza.Ushindi huo pia umeongeza kasi ya
ushindani baina ya Uruguay na Italy watapokutana Juni 24, ambapo wote walishamchapa
Uingereza, na wote wamechabangwa na Costa Rica, na ushindi wowote baina yao
utampleka aliyeshinda hatua inayofuata. Ila Italy ndiyo yenye matumaini zaidi
kwani ina magoli zaidi.... .jpg)
.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...