Mwili wa Marehemu George Tyson (pichani) utapelekwa nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach (eneo la Makonde) jijini Dar es salaam leo Jumanne Juni 3, 2014  kuanzia majira ya saa kumi jioni kwa ajili ya kuaga. 
Mwili utakuwepo nyumbani hapo mpaka siku ya Jumatano Juni 4, 2014 ambapo mwili utapelekwa kwenye viwanya vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es salaam,  kwa ajili ya shughuli ya kuaga mwili na ibada fupi.
Baadae mwili utapelekwa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere tayari kwa kusafirishwa kwenye jijini Nairobi nchini Kenya kwa mazishi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa 
kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2014

    tumwombe mungu, haya tunayoyaona yasiendelee, bali atupe kibali cha kuishi miaka iliyopo ndani ya biblia,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...