NI FURAHA TELE. Mwalimu wa kozi fupi wa Chuo
cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bi.
Bertha Ogwal, kushoto, akimkabidhi Bi. Jamila Mwenda, ripoti ya mahudhurio ya
kozi ya awali ya usekretari/kompyuta, hivi karibuni. Jamila ni miongoni mwa
vijana 11 toka mikoa mbalimbali nchini waliofadhiliwa masomo na shirika lisilo
la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), lenye
makao yake Marekani, ambalo linayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya
visima, maktaba za kijamii na ufadhili wa masomo ya ufundi. (Picha zote na
Nathan Mpangala wa HUC).
Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng’andu wa pili toka
kushoto, akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya ufundi magari, Yasini Musa hivi
karibuni. Yasin ni mmoja wa vijana waliopata ufadhili toka shirika lisilo la
kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC). Wengine katika picha
ni Msajili wa kozi Bi. Violet Fumbo na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Kozi
fupi Bw. Rocky Mongi.
Kijana Joseph Mboya (kulia) akilamba ganda lake
la ufundi magari toka kwa Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na
Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng’andu, jijini Dar es Salaam hivi
karibuni.
Mwalimu wa Umeme wa magari wa Chuo cha Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Saidi Mbwana,
akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya umeme wa magari, Bi. Neema Bungara
jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Neema ni mmoja wa vijana 11 waliopata ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika
lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
HAKIKA WAKIWEZESHWA WANAWEZA. Bi. Neema Bungara
akionesha ganda lake lililosheheni ‘A’ tupu. Neema ni mmoja wa vijana 11 waliopata
ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika lisilo la kiserikali la Help for
Underserved Communities Inc. (HUC).
ZAIDI BOFYA LINKS HIZI HAPA CHINI.
ZAIDI BOFYA LINKS HIZI HAPA CHINI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...