Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
 Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama
 Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
 Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
 Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hawa wahuni wameandaliwa na yule 'msaliti' a.k.a popo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2014

    Si walishaunda ACT,waache CHADEMA hakuna mgogoro wowote ni Njaa na kutumiwa ILS timing yao bite kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...