Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakigombania kulipa nauli kwa ajenti wa Basi la Urafika linalofanya safari zake kuelekea Iringa baada ya baadhi ya Vyuo kufungwa kwa pamoja na hivyo kufanya idadi ya abiria wa mikoani kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.
Baadhi ya abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma kufungwa kwa wakati mmoja.
Na John
Banda, Dodoma
DODOMA
imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani kutokana na vyuo
vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi kimoja hali
iliyowasababishia abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja na nauli kupanda kinyemela. Wanafunzi
hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), Mtakatifu Yohana, Mipango
na Maendeleo Vijijini (IRDP) na kile cha Biashara (CBE) ambavyo vina
wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.
Wakiongea na
mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika kituo cha mabasi ya
kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu kuusotea usafiri huo
bila mafanikio. Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote
kukutana kwa pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo
ya mabasi.
Hali
iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei kinyemela mpaka
kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi hicho huandikiwa nauri
ya kawaida tofauti na hapo hakuna anaesikilizwa.
‘’Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na
usafirishaji vinatakiwa kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii
ambayo vyuo vinafungwa ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama
tutondoka au la’’,
alisema
Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka
kuandikwa majina yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana
na siku za kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki
nzima. Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni
hapo alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi
imegwanyika katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na
17,000 la
tatu. Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela
alisema hilo wanalo na wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa
elimu ili wasilipe zaidi ya nauri iliyowekwa halali.
Wadau wa usafiri wanapaashwa kutarajia matukio haya ya kuongezeka kwa mahitaji ya usafiri ili waongeze huduma. Kungojea usafiri siku tatu humu nchini hakukubaliki anayekewnda ulaya anakuwa amefika na kuridi wewe huko nchi moja unahaha usafiri? halafu tunalalamika biashara haijashamiri!. tuchangamkie fursa.
ReplyDelete