Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge Mgimwa kwa uchapa kazi wake |
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE
wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema
atahakikisha anafanya kazi na vyama vyote vya siasa na kuwa
kuwataka wananchi wa jimbo la Kalenga kuachana na makundi ya vyama
vya siasa na kuunagana pamoja ili kufanikisha jimbo hilo kupiga
hatua kubwa ya kimaendeleo.
Mbali ya kuwataka
kuachana na makundi ya kisiasa pia amewataka waliokuwa wagombea wa
nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo kupitia CCM kuacha kujipitisha
kwa sasa kwa wananchi na badala yake kusubiri uchaguzi mkuu mwaka
2015.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika
mikutano yake ya hadhara kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa
kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge huyo alisema kuwa
amelazimika kuomba ruhusa
bungeni kwa spika ili kurudi kuwashukuru wananchi hao hasa
kutokana na upendo mkubwa ambao wananchi wa jimbo hilo walionyesha
kwake.
"Ndugu zangu nilianza kuzunguka katika
baadhi ya maeneo na kutekeleza ahadi mbali mbali hata kabla ya
kuapishwa rasmi bungeni ......na nitajitahidi kulingana na uwezo
wangu ili kuona natimiza wajibu wangu kwenu na kamwe sitawaangusha
ndani ya bunge na nje ya bunge"
Hivyo
aliwataka wananchi kwa umoja wao kuendelea kumuombea afya njema
ili kufanikisha kutimiza ndoto yake ya kufikisha maendeleo katika
jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutimiza sehemu kubwa ya ahadi ambazo
zilitolewa na marehemu Dr
Wiliam Mgimwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.
Kuhusu
suala la kuyawezesha makundi mbali mbali Mbunge Mgimwa aliwataka
wananchi kujiunga na vikundi vya VICOBA ili kuviwezesha vikundi
hivyo kiuchumi zaidi badala ya kuwa mtu mmoja mmoja na kuwataka
wazee pia kuanzisha umoja wao na kupeleka mahitaji yao katika
ofisi yake.
"Kuna vikundi vya VICOBA
ambavyo tayari vimeanzishwa na moja kati ya vikundi hivyo tayari
nimechangia kiasi cha Tsh 500,000 na nitaendelea kuchangia na kuna
eneo ambalo marehemu mbunge wetu aliyepita aliahidi kuchangia milioni 1
katika kikundi cha VICOBA Magubike nasema fedha hizo
nitazitoa mimi "
Alisema kuwa tayari
ameanza kupigania suala la umeme na maji katika vijiji vya jimbo la
Kalenga bungeni na kuwa mawaziri wa wizara hizo wameahidi
kulifanyia kazi na kuendelea kusaidia miradi hiyo mikubwa ambazo ndizo
ahadi kubwa zaidi.
Awali wananchi wa kijiji
cha Magubike walimpongeza mbunge huyo na kuwa katika historia ya
jimbo la Kalenga hawajapata kuwa na mbunge mkweli na mchakakazi kama
huyo na kurudi mapema zaidi kwa wananchi kuwashukuru na hivyo
kumhakikishia kuwa hawana mpango wa kumchagua mbunge mwingine mwaka
2015 na kukiomba chama cha mapinduzi kumbariki kuendelea kuongoza jimbo
hilo .
Kwa upande wake katibu mwenezi wa CCM
wilaya ya Iringa Denis Lupala alisema kuwa utendaji kazi mzuri wa
mbunge huo ndio ambao unakishawishi chama kuendelea kumpa ushirikiano
zaidi na kuwa wananchi hawana sababu ya kubabaishwa na wapinzani ambao
wameanza kujipitisha katika jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...