Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents wakipewa maelekezo ya jinsi magazeti ya kampuni hiyo yanavyoandaliwa hadi yanaponunuliwa na wadau wa habari
Maelekezo yakiendelea kwa washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents
Washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publisher mara baada yakutembelea ofisi zao leo zilizopo
Bamaga Mwenge Jijini Dar Es Salaam.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
Washindi wa Kanda zote Sita za Tanzania wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washiriki wa Fainali ya Shindano hilo kubwa kabisa nchini na Afrika Mashariki na Kati watembelea ofisi za Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Risasi, Ijumaa, Uwazi nk ya Global Publishers limited kwaajili ya kujionea jinsi magazeti kutoka kampuni hiyo yanavyoandaliwa mpaka yanapowafikia wasomaji.
Washiriki hao pia waliweza kupata fursa ya kuuliza maswali kwa wafanyakazi hao wa Kampuni ya Global Publishers kwaajili yakufahamu mambo mbalimbali yanayohusu kampuni hiyo Kubwa kabisa Tanzania.
Washiriki wa Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wanatarajia kuingia kambini leo tayari kwa mchakato wa kushindania shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa mshindi mmoja.
Huu ndio muda wa Watanzania kuweza kumchagua mshindi wa Milioni 50 kwa kumpigia kura mshiriki ambae ataonekana kukuna nyonga zao kwa kuonyesha kipaji cha kweli. Watanzania wataweza kuwapigia kura washiriki watakaoonekana kuwa na vipaji kwa kutuma namba za washiriki kwenda namba maalumu itakayotolewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...