Na Abdulaziz Lindi
Watu watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja
kuacha njia na kupinduka na kufasabisha vifo vya watu hao na kujeruhi
wengine wawili katika ajali iliyotokea Jana Huko Tarafa ya Rondo
wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.
Ajali hiyo Iliyohusisha gari aina ya HOWO lenye Usajili T270BZU na
Tela na T260AZU Pamoja na Lori aina HOWO T871 BTH Tela T 626 BTT yote
yaliacha njia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi kamishna msaidizi Renatha Mzinga
amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao ambao ni
Marehemu Jackson Francis Kayombo (DEREVA) mwenye umri wa miaka
42,marehemu Lazaro Michael Chaula,(Mkinga) miaka 27 Dereva na Marehemu
Mohamed Jumanne Said (Mmakonde) miaka 23.
Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni ambao ni
Given Mussa Mohamed na Seleman Ibrahim Hamis ambapo pia alibainisha
kuwa Maiti na majeruhi wote wamefikishwa katika Hospital ya Sokoine
Manispaa ya Lindi.
Aidha kamanda Mzinga pia alieleza matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo
Wakazi wanne wa wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Manispaa ya Lindi,
wamefariki dunia katika matukio tafauti,likiwemo mtu anayesadikiwa
kuwa na matatizo ya akili kuwapiga vikongwe wawili mwishoni mwa wiki
iliyopita mkoani hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...