Na Allan Ntana, Tabora
IMEELEZWA kuwa tunu ya amani na utulivu iliyohapa nchini ni matokeo ya
maombi ya wacha Mungu yanayofanyika katika nyumba za ibada kila
iitwapo leo pasipokukoma.
Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu
aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa katika sherehe za
Jubilee ya Miaka 75 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)
zinazoendelea katika majimbo yote ya kanisa hilo hapa nchini.
Kingu alisema katika ibada maalumu iliyofanyika katika uwanja wa ofisi mpya za jimbo mjini Tabora kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia
sana mchango wa kanisa katika kudumisha amani, mshikamano na utulivu
wa Watanzania kupitia maombi kwa kuwa Mungu anasikia maombi yao.
‘Ndugu zangu wana TAG, serikali inatambua sana mchango wenu katika
kudumisha amani na utulivu wa nchi hii, nina amini kama makanisa
yangekuwa hayaombei taifa, amani ya nchi hii isingekuwa kama ilivyo
sasa, machafuko yangekuwa mengi zaidi’, alisema.
Aliwataka watumishi wa Mungu kote nchini kupitia ibada zao au mikutano
ya hadhara kuisaidia serikali kukemea vitendo vyote vinavyoashiria
uvunjifu wa amani au baadhi ya watumishi wa umma kutumia madaraka yao
vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa mali ya umma. "Kanisa ndilo jicho la nchi, watumishi wa Mungu mkisimama imara
mkamlilia Mungu maadui wote wanaoitazama nchi hii kwa jicho la husuda
huku wakitamani kuvuruga amani iliyopo, hila zao za chokochoko na
mauaji hazitafanikiwa kabisa, aliongeza.
DC Kingu aliwataka watumishi hao kuwa na maadili mema katika utumishi
wao huku akionya wale wote wenye nia ya kuligawa taifa katika misingi
ya udini kuwa nia na dhamira zao hazitafanikiwa kwani serikali ipo
macho na wote wenye nia hiyo watashughulikiwa mara moja.
Aidha DC Kingu alimshukuru Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dr Barnabas
Mtokambali na waumini wote wa kanisa hilo hapa nchini kwa moyo wao wa
upendo wa kuwajali na kuwasaidia wagonjwa na wanajamii walio katika
mazingira magumu sambamba na kujali usafi wa mazingira.
Wakati huo huo kanisa la Tanzania Assemblies of God hapa nchini limetenga jumla ya sh mil.270 kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali ya kijamii katika sherehe za maadhimisho ya Jubilee ya kanisa hilo hapa nchini.
Hayo yalibainishwa jana na Askofu Mkuu wa kanisa hilo hapa nchini Dr Barnabas Mtokambali katika ibada maalumu iliyofanyika katika uwanja wa ofisi mpya za jimbo mjini Tabora.
Alisema katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini kanisa limeandaa kiasi cha sh milioni 270 kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa makundi ya watu mbalimbali wenye uhitaji.
Dr Mtokambali alifafanua kuwa watatoa vyandarua, damu na vitu mbalimbali kwa jamii ya watanzania wenye uhitaji pasipo kujali dini ya mtu, rangi wala kabila, lengo likiwa ni kumshukuru Mungu kwa kuliwezesha kanisa hilo kutimiza miaka 75.
Alisema sherehe za maadhimisho ya Jubilee ya kanisa hilo lililoanzishwa mwaka 1932 hapa nchini na sasa likiwa na waumini zaidi ya milioni 5 tayari zilishaanza katika makanisa ya TAG hapa nchini na zinaendelea katika majimbo yote 32 ya kanisa hilo.
Kilele cha maadhimisho hayo ya kihistoria yatakayohudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo maaskofu , wachungaji, viongozi wa taasisi, mashirika, dini mbalimbali, viongozi wa serikali na wananchi kitakuwa tarehe 13 Julai 2014 jijini Mbeya na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema.
Awali askofu wa jimbo la Tabora Paul Meivukie alimweleza Askofu Mkuu Mtokambali kuwa wameazimia kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuanzisha vituo 2 vya kuhudumia watoto yatima katika wilaya za
Sikonge na Uyui, tayari vimeanza kazi. Mradi mwingine ni mradi wa kufyatua matofali ya kuuza (interlock) mashine yenye uwezo wa kufyatua tofali 1000 kwa siku moja tayari imenunuliwa na ujenzi wa kituo cha jimbo la Tabora nao tayari umeanza.
Miradi inayotarajiwa kuanzishwa ni pamoja na ujenzi wa Chuo Kikuu cha
Wachungaji, ujenzi wa shule 2 za sekondari, uchimbaji visima 3 vya maji na ujenzi wa kituo cha afya katika eneo la Ipuli katika manispaa ya Tabora.

Mkuu wa wilaya ya Igunga Mhe. Elibariki Kingu aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akiongea katika sherehe za Jubilee ya Miaka 75 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) katika ibada maalumu iliyofanyika katika uwanja wa ofisi mpya za jimbo mjini Tabora.
Mhe Kingu akishukuru baada ya kupokea misaada toka kwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo hapa nchini Dr Barnabas Mtokambali (mwenye fulana ya hudhurungi) katika sherehe za Jubilee ya Miaka 75 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) katika ibada maalumu iliyofanyika katika uwanja wa ofisi mpya za jimbo mjini Tabora leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...