Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyata International Convention Centre hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya. Kushoto kwa Rais Kenyata ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Mheshimiwa Kyriakos Gerentopoulos. Ujumbe wa Tanzania ulishirikisha pia Mhe. Janet Mbene (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (aliyevaa gauni la kijani).

 Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akimshukuru Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre jijini Nairobi, Kenya.



Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), na Rais wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Carribean na Pacific akiongoza Mkutano wa 99 wa Baraza hilo la Mawaziri. Kushoto kwake ni Mheshimiwa Adan Abdulla Mohamed, Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya akifuatilia mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre, Nairobi Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...