Nguli wa Maswala ya Uongozi na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy kutoka nchini Marekani,Brian Tracy akikiongoza semina maalum ya uongozi bora iliyoandaliwa na Mikono Speakers,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Nguli mwingine alietoa mada kwenye Semina hiyo ni Azim Jamal ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.
Sehemu ya Wadau kutoka nyanja mbali mbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Semina hiyo iliyoongozwa na Manguli wa Maswala ya Uongozi Duniani, Brian Tracy na Azim Jamal,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wakifatilia kwa makini Mada mbali mbali kwenye semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...