"Ohoooooo.... Gari langu maskini...." Dereva wa teksi anatoka nje kuangalia jinsi gari lake lilivyoingia kwenye chemba ya maji machafu ambayo mfuniko wame umeeshaenda kusikojulikana na kuacha shimo kubwa katikati ya barabara ya Mtaa wa Zanaki jijini Dar es salaam leo
Wasamaria wema wanasogea kuja kumuokoa
"Hayaaaa....twendeeeeee" Gari linatoka
Anapiga rivasi taratibu huku mshimo ukiwa umeachama
Anaondoka taratibu huku akisikitika na kujiuliza nini kifanyike kuondoa adha hii jijini....
Yaani huyu dereva hakuliona hilo shimo??
ReplyDeleteWahusika watafute mifuniko mbadala kama ya zege badala ya chuma kuondokana na hii kero
ReplyDeleteAma kweli hii dunia ina tofauti kubwa kati ya nchi na nchi. Shimo kama hili lingeoneka huku nchi za wenzetu basi angeshitakiwa mkuu wa jiji lakini huko kwetu linaonekana kama ni jambo la kawaida sana na dereva anaondoka kama hakuna kitu kilichotokea.Any way kidogokidogo nasi tutafika tu oneday
ReplyDeleteHuyo mdao hapo juu anikumbusha mbali sana. maana miaka hiyo niliwahi kutumbukia kwenye shimo kama hilo, na gari langu likapata uharibifu kweli. Kisha nikazungukwa na wajanja, mmoja wao takribani miaka mitano ama sita hivi, kisha kajaa mafua, akaniambia, hukuliona hilo shimo, wewe kipofu nini.He just made my day.
ReplyDelete