Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.

Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.

Katika miaka hiyo zao la karafuu lilikuwa ndiyo tegemeo kubwa la pato la kiuchumi katika visiwa vya Zanzibar.  Pato la Serikali lilitegemea sana zao hilo na kuiwezesha kuenedesha mipango yake ya kiuchumi na kijamii bila ya kuyumba. Hali hiyo ilitokana na ukubwa wa soko la dunia na ubora wa kipekee wa karafuu za Zanzibar katika soko hilo.

Lakini kwenye miaka ya 1990, hali ya soko haikuwa nzuri sambamba na kushuga kwa bei na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha karafuu duniani na hivyo kuleta ushindani wa kibiashara.

Kushuka kwa bei katika soko la dunia kulipelekea kushuka kwa ari ya  uzalishaji kwa wakulima na kupelekea visiwa vya Zanzibar navyo kupoteza muelekeo wa zao hili. Zao hili lilipoteza hadhi yake ya kuwa zao la uchumi wa nchi.


Wakulima wengi waliacha kulima zao la karafuu na badala yake walijihughulisha na mazao mengine ukiwemo ukulima wa mwani ambapo wakati huo ulionekana kama ungelikuwa mbadala wa zao la karafuu.

Lakini pamoja na kuyumba kwa soko la dunia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliendelea kununua karafuu kutoka kwa wakulima, ingawa si kwa bei ya kiwango cha juu. Serikali ililazimika wakati mwengine kufidia gharama za bei katika kuona mkulima ambaye ni mwananchi anaendelea kujenga imani na kulithamini zao la karafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...