Leo
majira ya saa kumi alfajiri kumetokea ajali ya maporomoko ya mawe katika eneo
la juu la Mlima Kilimanjaro la Hans Meyer na kusababisha kifo kwa mwanafunzi
Malata Thomas kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli .
Aidha,
mwanafunzi mwingine Matenga S.J alivunjika mguu wake na anaendelea na matibabu
katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.
Wanajeshi
hawa walikuwa pamoja na wenzao 265 walikuwa katika mafunzo yao ya kawaida ya
ukakamavu katika Mlima Kilimanjaro.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linaendelea na taratibu za kufahamu chanzo cha kutokea kwa
ajali hiyo na taarifa kamili itatolewa kwa umma mara baada ya kukamilika.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
15.07.2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...