Mkali
wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime
anatarajiwa kutoa burudani kali hapo August 2, katika ukumbi wa Golden
Tulip jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo linaloandaliwa na kituo cha Radio 5 litaambatana na burudani ya
muziki kutoka ODAMA Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka
Kenya na Pilipili wa Tanzania.
Akizungumzia
tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis
alisema kuwa wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali
ya juu katika uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.
“Kansiime
ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa
uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.
Kansiime
amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa
kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana
na changamoto mbalimbali za maisha.
Mchekeshaji
huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With
Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye
kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Burudani
hii ya Kansiime, ambayo itakwenda kwa jina la Cheka Kwa Nguvu, itaanza
saa moja usiku na tiketi zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na
shilingi 700,000 kwa meza ya watu nane.
‘Kama
ambavyo mwandishi wa vitabu, Maya Angelou alivyowahi kusema, “Simwamini
mtu yeyote asiye cheka” tukio hili linalenga kuonesha umuhimu wa
kucheka katika maisha yetu ya kila siku” alihitimisha Francis.
tumwombe Mungu atupe uzima, nampendaga huyu mdada! mbona kiingilio kikubwa hivyo?
ReplyDeletedada namkubali sana na I wish to there...lkn kiingilio kimekuwa kikubwa na ukichukulia watu watakuwa wametoka kwenye shughuli ya Idd...waandaaji yawabidi mwangalie mwenendo wa hela kwa mji huu.
ReplyDelete