Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akishukuru Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EIB) kwa kutoa  mikopo ya gharama nafuu na kusaidia Maendeleo ya nchi za ACP. Balozi Kamala ameitaka Benki hiyo kuongeza kiwango cha mikopo inayotoa katika nchi za ACP kutoka asilimia 10 ya mikopo inayotoa sasa hadi asilimia 20. 

Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP leo imekutana na Uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ulaya, Luxembourg kubadilishana mawazo jinsi ya kuboresha utendaji wa Benki na kuweka vipaumbele vya maendeleo na ushirikiano kati ya nchi za ACP na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...