Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Namikango, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi leo. 
Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo kila mwanachama wa chama hicho alisisitizwa kuchukua fomu wakati muda utakapofika wa kuchukua fomu hizo. 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wananchi watachagua Viongozi wa Mamlaka za Wilaya, Mamlaka za Miji midogo, Mamlaka za Miji na Halmashauri za Vijiji na Vitongoji. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Albert Mnali. Picha na Felix Mwagara wa WMNN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...