Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya
Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.
WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.
Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.
PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO
Wamuulize...pengine ana wito jamani...zamani...mapolisi, madakatari waalimu hata wanajeshi, wahusika walikua wakipatikana kwa njia kama hizi za kujisogeza tu na eneo la tukio kwa mapenzi ya dhati....kisha kupewa ajira....ushauri wangu wasikimbilie kumpeleka polisi....
ReplyDeletenakuunga mkono sana mtoa maoni ya kwanza,nilitaka kucomment hivyo huyo ana wito na sio wa kumpuuza anaweza kuwa mganga mzuri sana. kwanza ana umri mdogo wamchunguze kwa busara..
ReplyDeleteIt is very serious offense, don't play with people's lifes
ReplyDeleteNaungana na wewe |Anony 1 and 2; nisikia kwenye vyombo vya habari kuwa alitaka kuwasaidia wagonjwa! Nahisi asipuuzwe kwani hao madaktari na manesi wamezidi kulingia wagonjwa na hata majuzi tulisikia kule Muheza wananchi wakilalamikia dharalau zao. Ndio wajue wapo watu mtaani wanao uwezo wa kufanya hizo kazi. I don't believe with you Anony 3, kwamba asicheze na maisha ya watu; kama wewe ni daktari habari ndio hiyo!!! Ninyi madaktari na manesi mbona mnapokwenda kufanyakazi private hosp. mbona hamnyanyasi wagonjwa kama mnavyotenda kwenye hospitali za Umma!!!
ReplyDeleteKama huyo kijana ana passion angeomba kwenda chuo kidogo ambacho baadaye angeendelea kuwa daktari au angejitolea hospitalini kuwasaidia wagonjwa lakini si
ReplyDeletekujifanya daktari na kuvaa koti jeupe wakati hana taaluma hiyo na kuhatarisha usalama
wa wagonjwa. Nahisi huyo kijana alitaka
kuchukua rushwa kwa wagonjwa kama ilivyo
sasa kuna wimbi kubwa la watu hasa vijana kujifanya madaktari, polisi na vyeo vingine. Haiwezekani kunakuwa na mianya namna hii na watu wengine wanashabikia wakati maisha ya wagonjwa na wananchi wasio na kosa yanahatarishwa na hao wahuni na wazembe ambao maisha yamewashinda.