Anuary Mkama kutoka Radio Mlimani nchini Tanzania na mwenzake Amida Issa kutoka Burundi waagwa rasmi DW mjini Bonn baada ya kumaliza mafunzo utangazaji kwa vitendo yaliyodumu katika kipindi cha miezi sita. Wote wawili sasa wanajiandaa kurejea katika mataifa yao kwenda kutuma ujuzi waliouvuna kutoka DW Bonn.
Wafanyakazi wa DW baada ya hafla fupi ya kuwaaga watangazaji Anuary Mkama kutoka Tanzania na Amida Issa kutoka Burundi.
Anuary Mkama akikabidhiwa cheti chake na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Mohammed Abdulrahman baada ya kupata mafunzo ya utangazaji kwa vitendo kwa miezi sita.
Kutoka kushoto Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Mohammed Abdulrahman, Amida Issa, mtangazaji mkongwe Sekione Kitojo "Seki" na Anuary Mkama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...